
Psalm 23
Amapianogospel
Verse 1 Bwana ni mchungaji wangu, Sitapungukiwa kitu. Hun'laza penye majani mabichi, Huniongoza kwa maji matulivu. Chorus Hakika wema nazo fadhili Zitanifuata mimi, Nitakaa nyumbani mwa Bwana, Siku zote za maisha yangu. Verse 2 Hunihuisha nafsi yangu, Hun'ongoza kwa njia za haki. Nipitapo bondeni mwa mauti, Sitaogopa wewe u nami. Chorus Hakika wema nazo fadhili Zitanifuata mimi, Nitakaa nyumbani mwa Bwana, Siku zote za maisha yangu. Verse 3 Gongo lako na fimbo yako, Vitanifariji mimi. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Chorus Hakika wema nazo fadhili Zitanifuata mimi, Nitakaa nyumbani mwa Bwana, Siku zote za maisha yangu.